Saturday, June 1, 2013

PICHA ZA MAANDALIZI YA MSIBA WA NGWEA..TAZAMA KINACHOENDELEA MPAKA SASA

 

 
 
 
 
 

MAOMBOLEZO ya msiba wa aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea, yameanza  nyumbanmi kwa baba yake mdogo, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako jana jioni ndugu, jamaa na majirani walikutwa wakiwa katika matayarisho ya kuupokea mwili wa marehemu.

Friday, May 31, 2013

DIAMOND AENDELEA KUMUOMBA MSAMAHA JOKATE

source HYPERMAN HK
Na Imelda Mtema
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.
...Diamond na Jokate wakicheza.
“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline  Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.
PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”Chanzo:www.globalpublishers.info

PUMZIKA KWA AMANI DEAR BROTHER GWEA

Rest in peace mwana chemba. MIMI kama CANDY CALFONIA napenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jirani, marafiki,shabiki na watanzania wote kwa kuondokewa na nguvu au mchango uliodumu kwenye game kitambo, kifo kinatukumbusha kusafisha njia zetu na kuishi kwa kupendana tukikumbuka kua siku yoyote mtu yoyote anaweza anguka haijalishi tajiri, maskini, au maarufu, poleni ana na tusichoke kumuombea ndugu yetu pia natoa hongera na shukran kwa wooote walio changia na wanaoendelea kuchangia chochote juu ya msiba huu,, TULIKUPENDA, ULITUPENDA,ULITUBURUDISHA , ULITUJARI LAKINI ALIEKUUMBA KAKUPENDA ZAIDI YA SISI,
I WL ALWYZ REMEMBER YOU GWEA. GO ITS UR WAY...........AMENI
Inasemekana ndugu yangu kumbe ulikuwa na mengi ya kuongea kutoka moyoni mwako lakini ukutaka kusema, sasa sijui linaukweli ili maana atuna uwakika na iloLeo umeondoka yanazungumzwa mengi sana,mara ili mara lileBaada ya watu tukuombee ndugu yangu kwa kipindi iki,uku tukijadili jinsi gani tunaweza kukurudisha katika Taifa lako na kwenda kukupumzisha katika nyumba yako ya mileleTunaongelea mambo ambayo kwasasa hayana faida,kitu ambacho kilitakiwa kiongelewe kipindi wewe upo haiSema mimi nawaambia kupitia hii status yangu kama kweli wanauchungu na wewe,iki ni kipindi ambacho wanatakiwa kusimamia kazi zako,kama watasimamia vizuri kazi zako naamini malaika wako uko walipo watafurahiAnasema stress ndizo zilizo kuingiza kwenye utumiaji wa madawa,kama kweli ulimwambia matatizo yako swali la kujiuliza, alitumia njia gani kuhakikisha anakutoa katika ile hali ya stress?


Au kwasababu leo umetutoka ndio tunapata nguvu ya kuongea,kitu ambacho kwasasa akisaidii?Na sema ivi huu ni wakati wa kumwombea marehemu,kushirikiana na kuakikisha tunamrudisha katika Taifa lake tayari kwa kumpumzisha katika nyumba yake ya mileleKuna haja ya kutengeneza ulingo wa ngumi kwa watu wenye bifu,kama watashindwa kuelewana kisheria,kwa kurushiana maneno,muwe mnamalizana kwenye izo ulingo kwa kuchapana makonde....!!@TeamYamoyoni

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 31.05.2013 VICHWA VIKUBWA LEO WALIOPATA 0 FORM 4 WAPETA,HOTUBA YA USHOGA YATIKISA BUNGE NA WANAFUNZI WAUAWA KINYAMA.

source dj sek

2 fdb2c
3 150c8
4 febf0
5 5e5ed
6 67f92
7 2a87d
9 e2ad8
10 cfcf1
11 5ff32
13 c0ecb

Friday, March 22, 2013

HIKI NDICHO KILICHOMPATA LINEX BAADA YA KUMCHUMBIA MZUNGU


SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ kumvisha pete ya uchumba demu wake mtasha, Suvi Rikka, mama wa staa huyo, Imelda Barnabas ameibuka na kumchana mwanaye kuwa haitambui pete wala mchumba huyo kwa kuwa kitendo hicho hakina baraka zake wala za familia.
 
Sunday Mangu ‘Linex’ akiwa na mchumba wake Suvi Rikka.
Linex alipoulizwa juu ya sakata hilo, alifunguka:
“Yah! Bi mkubwa amenijia juu ile mbaya, ila najitahidi kumuomba msamaha, hope atanielewa.”


Source : Global Publishers

BREAKING NEWS!!! CHINUA ACHEBE AFARIKI DUNIA


 
R.I.P Chinua Achebe.

Mwandishi mkongwe wa vitabu toka nchini Nigeria. Prof. Chinua Achebe amefariki dunia akiwa nyumbani kwake huko nchini Marekani alipokuwa akiishi akifundisha Brown University .

Prof. Chinua Achebe ambaye amefariki akiwa na miaka 82 inasemekana hivi karibuni amekuwa akihudhuria hospitali mara kwa mara kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua ila hajawekwa wazi.

Vitabu alivyowahi kuandika ni Things Fall Apart, A Man of the People, Arrow of God, No Longer at Ease na Anthills of the Savannah.

Sunday, March 17, 2013

KIJANA ALIYEANDAA VIDEO YA LWAKATARE NAYE ATIWA MBARONI....NDIO HUYU HAPA


 

Anayedaiwa  kupiga  video  iliyosababisha   kukamatwa kwa  Rwakatale (  pichani ) maarufu kwa jina la  Ludovik Joseph amekamatwa  mkoani Iringa .kijana   huyo anadaiwa kuwa ni mhitimu  wa  chuo kikuu cha DUCE

-------------------------------- Ndugu zangu,
Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.


Namfahamu kijana Ludovik tangu  akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi  walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini.


Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi  kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. 


Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii. Amekuwa na mchango mkubwa, na hata katika miezi ya karibuni,ndiye yeye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti  kwenye Mjengwablog kila asubuhi.

 Akiwa Dar na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali , amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice kwa watangazaji kwenye Mjengwablog.

Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti'.

Na jana nilimwomba aje Iringa aniletee vitabu vyangu vya invoice na risiti kwa vile nilitarajia ugeni wa kutoka TMF- Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari. Kwamba huenda vitabu hivyo vingehitajika wakati wa mazungumzo  na watendaji wa TMF yaliyofanyika leo asubuhi.


Hata hivyo, katika hili lililomtokea, siwezi hapa kumtetea wala kumtia hatiani. Maana, naye ni binadamu kama wengine, siwezi kusema kuwa ninamfahamu sana.  Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama , nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima.


 Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo. 


Ni mimi:
MAGID MJENGWA