ABOUT ME


NILIHISI KUMPOTEZA MAMA YANGU NI MWISHO WANGU PIA. Mimi ni mtoto wakike wa pekee katika familia yetu yenye watoto watatu, mama yetu alitulea kwa upendo mkubwa saana japo alikuwa muajiliwa katika kampuni fulani lakini bado alifungua biashara zake zingine ili kuhakikisha wanae tunapata kila tunachohitaji ikiwemo na elimu bora, Nilipendwa sana na mama kwani nilikuwa napenda shule napenda kuimba na vile vile napenda kutembea nae popote furaha yake ilikuwa furaha yetu pia furaha yetu ilikuwa yake, nikiwa form3 niliweza kushiriki miss mapoz mbeya nilikokuwa nikisoma niliifanikiwa kushinda jambo hili mama hakulipenda coz alikuwa mtu wa dini nilijisikia vibaya kumuhuzunisha mama yangu kwani kipindi hicho alikuwa ni mgonjwa, mda ulienda akiwa bado mgonjwa na aligundulika na SALATANI YA KIZAZI alipelekwa OCEANROAD kwa matibabu baada ya mda alipona na kuwa mzima maisha yakaendelea, mda ulipita ugonjwa wake ukarudi tena safari hii mama alikuwa hajiwezi kwa lolote ndugu walijitahidi kumuuguza lakini haikuwa mipango ya mungu bahati mbaya alifariki, tangu nimezaliwa hili swala lilikuwa zito saana kulikubari ikafika kipindi nikawa sijielew kama napoteza faham then zinanirudia,, kwa rehema za mungu nilifanikiwa kumaliza olevel na kuendelea na Alevel nikiwa nimekata tamaa vitu viNgi vilibadilika maisha pia hayakuwa na furaha kama mwanzo nilikuwa ninandugu wengi ila sina mtu wa karibu kama alivokuwa mama yangu nikawa navunjika moyo saana nakata tamaa, kunamda nilikuwa nasema hivi hata nikisoma nikiwa na pesa yangu faida gani ntapata wakati niliepaswa kufurahi nae hayupo,,enzi za uhai wake alipenda muziki saana na aliimba nyimbo za dini, hivo kufanya kwangu muziki ni kama kumuenzi mama yangu kwani sasa nimeamua kusomea kabisa muziki ili kuzidi kumfurahisha japo hayupo tena nami,, ningepata hata dk 1 ya kumuona tana nahis ningemueleza meengi japo kwa mda mchache angejua hisia zangu na jinsi gani bado nampenda saans napia ningemueleza mengi kuhusu muziki wangu,, hii ndio ilikuwa safari ya maisha ya mama yangu mpenzi SUSSAN JACKSON.

 AHSANTENI

5 comments:

  1. Very painful...pole sana

    ReplyDelete
  2. Be strong in wateva u do n will alwyz b with u.

    ReplyDelete
  3. ooooh pole sanaaa but usichoke kuimbaa sawaee,na mm nitakusaidia coz naweza kutunga but sina sauti ya kuimbaa sawaee kama ukihitajii


    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO HAPA