Friday, January 25, 2013

HIVI NDIVYO PARTY YA KUUKARIKBISHA MWAKA YA CLOUDS MEDIA GROUP ILIVYOKUWA, TAZAMA PICHA



Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana usiku wa kuamkia leo kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.
Boss Joe akiwaomba wafanyakazi wote wazinyanyue glassi zao za vinywaji juu na kuzigonganisha kwa pamoja kuonesha upendo,mshikamano na ushirikiano.Baada ya hapo Wafanyakazi walipewa ruksa ya kula kunywa na kujimwaya mwaya.
 Shampeni ikimiminwa baada ya kufunguliwa.
 Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo.
 Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.
Dj Zero akiangusha ngoma live ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2 usiku wa kuamkia leo.
Baadae wafanyakazi wa Clouds Media Group walianza kupata chakula cha pamoja kama uonavyo pichani. 
  Kulia ni Paul James a.k.a PJ,Suka,Dj Steve B pamoja na Dj Peter Mo wakipata msosi huku wakibadilisha mawazo usiku huu ndani ya kiota cha Escape 2
 Dj Mayanga akiangusha ngoma za kufa mtu usiku huu ndani ya Escape 2
 Pichani kulia ni Dj Venture,Gerald Hando pamoja na Mdau mwingine.
 Kulia ni Dj Too Shot,Dj Bulla akiw ana Mdau kimapozi ndani ya picha.
 Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Paul James a.k.a PJ akifurahia jambo na Meneja vipindi wa clouds FM,Sebastian Maganga usiku huu ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2. 
 Dj PQ aliyekaa wakipiga stori na sebastian Maganga pamoja na PJ.
Mzee wa Kipindi Cha Jahazi,Eprahim Kibonde na mdau mwingine wakipata vitu laini laini safi kabisa.
 Ilikuw ni full kujichana,kula kunywa na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya hafla usikuu huu ndani ya Escape 2.
 Dada Regina Mwalekwa akiwa amepozi na Bonge Barabarani.
 Cheersssss
 Pichani kulia ni mdau mkubwa wa Clouds Media Group,Dauda wa Kota akifurahia jambo na Dada Regina Mwalekwa.
 Sehemu ya kikosi kazi cha Clouds Tv wakishangilia jambo.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA