Thursday, January 31, 2013

TUNDA MAN : UMILIKI WA BASTOLA WAMTOKEA PUANI

TABIA ya baadhi ya mastaa kuonyeshaonyesha bastola hadharani kimemtokea puani ‘memba’ wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’ baada ya hivi karibuni kuitwa na jeshi la polisi na kuhenyeshwa.
 
Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’.
Akizungumza na GPL hivi karibuni Tunda Man alisema makala iliyotoka kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa Wikienda ikieleza jinsi baadhi ya wasanii wanavyozianika silaha kiholela imemfanya akione cha moto kwani wakati akizungumza na mwandishi wetu alikuwa Kituo cha Polisi cha Kati (Central) akihojiwa.
“Kwanza naomba nikwambie kuwa hakuna kitu ambacho kimenikosesha amani leo (Jumatatu) kama hii habari yako uliyoandika kwenye gazeti, hivi ninavyoongea na wewe niko ‘sentro’ nikihojiwa, kiukweli sina amani,” alisema Tunda Man.
Hivi karibuni msanii wa muziki, Aboubakar Chende ‘Dogo Janja’ alinaswa akiwa na bastola na alipoulizwa ni ya nani alidai ni ya Tunda Man hivyo kumpa msala mwenzake.

 SOURCE: GPL

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA