Saturday, February 16, 2013

ANGALIA PICHA ZA NAMNA WAENDESHA BODABODA WALIVYOFUNGA BARABARA MOROGORO



Waendesha pikipiki  maarufu kama bodaboda wamefunga barabara kwa muda  mkoani  morogoro.
Waendesha pikipiki  hao wamefunga barabaraya kutokea mjini kuelekea kituo kukuu cha mabasi msavu eneo la masika wakipinga utaratibu mbovu unaotumiwa na mamlaka ya kukusanya kodi mkoa wa morogoro (TRA) Wa kuwakamata waendesha bodaboda hao bila utaratibu,Akisumulia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda hao amesema TRA wameanza utaraibu wa kuwakimbiza waendesha pikipiki hao kwa kutumia magari jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Akiendelea amesema pia wamekuwa wakiwakamata kwa vurugu na bugudha kubwa bila kujali wapo waliolipa kodi na ambao hawajalipa kodi.
Moto uliowashwa na waendesha bodaboda hao waliofunga barabara mkoani morogoro kwa kuchoma matairi, kupanga magogo,na  mawe barabarani  kwa lengo la kuipinga  uwonevu unaofanywa na mamlaka ya kukusanya mapatoya kukusanya mapato mkoa wa morogoro dhidi yao.






Moto huo ukiendelea kuwaka kabla ya kudhibitiwa na jeshi la polisi mchana huu
Moto huo ukizimwa na kikosi cha zimamoto  mkoa wa morogoro baada ya kufuka eneo la tukio
wakazi wa morogoro wakiwa wamesimama kando ya barabara hiyo kushuhudia tukio hilo mchana huu mjini morogoro
Mkuu wa kituo cha polisi morogoro mjini akiwa eneo la tukio kuhakikisha usalama na amani unakuwepo baada ya  kufanikiwa  kudhibiti tukio hilo

SOURCE: DJ SEK

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA