Wednesday, February 6, 2013

FLAVIAN MATATA ALAMBA SHAVU LA MATANGAZO YA DIESEL + EDUN



Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.


Kampeni ya DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya DIESEL – Renzo Rosso – na waanzalishi wa kampuni ya EDUN – Ali Hewson na Bono walisafiri hadi nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa. 

Waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.

Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.

Mwanamitindo Flaviana Matata ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA