Waigizaji zaidi ya 30 ambao
jumapili february 3 2013 walijitokeza kumpokea mwigizaji mwenzao mgonjwa
Matumaini, walirudi mikono mitupu baada ya mwigizaji huyo aliekua
anatarajiwa kuwasili Tanzania akitokea Msumbiji kushindwa kufanya hivyo
chanzo kikiwa ni hati yake ya kusafiria ambayo akiwa uwanja wa ndege
aliagizwa kuishughulikia kwenye ofisi za uhamiaji ambazo zipo mbali na
uwanja wa ndege.
.
Matumaini amekua Msumbiji kwa
wiki kadhaa alikokwenda kufanya show lakini muda mfupi baadae mambo
yakageuka na kuanza kuumwa miguu, mwigizaji huyu anatarajiwa kuwasili
Dar jumanne au jumatano na tayari umoja wa waigizaji umepanga kumpeleka
hospitalini moja kwa moja.
Waigizaji waliokwenda kumpokea.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA