Saturday, February 16, 2013

HUU NDIO UGONJWA ULIOMUUA GOLDIE.......

Written By Tryphone Nyahinga on Friday, February 15, 2013 | 5:39 PM


Marehemu Goldie Harvey ambaye alikutwa na mauti juzi usiku kwenye mida ya saa tano kuwafanya mashabiki wake kushikwa na simanzi kubwa kuhusiana na taarifa za kifo chake imeelezwa kuwa ugonjwa wa ''Pulmonary Embolism'' ndio uliopelekea kifo chake.
Ugonjwa huo unaosababishwa na kuganda kwa damu, husababisha mshipa mkubwa ambao unasafirisha damu na hewa kwenda kwenye mapafu kuziba na kupelekea binadamu kufariki ghafla.
Goldie alifariki jana kutokana na ugonjwa huo akiwahishwa hospitali ikiwa ni muda mchache baada ya kuwasili jijini Lagos, Nigeria akitokea Los Angeles, America.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA