Saturday, March 16, 2013

HEMEDI : MIMI SIRINGI TOFAUTISHENI SWAG NA KURINGA

Baada ya kuwepo kwa maswali mengi kuhusu tabia ya mwanamziki na muigizaji Hemedi Suleiman a.k.a PHD, kuwa anaringa sana, na ni mtu ambae anapenda sana kuwa na watoto wa kike.
hiki ndicho alichokizungumza Hemedi leo hii kupitia xxl ya Clouds fm

"naomba jamani watu wajue kuwa mi siringi, ila watofautishe kati ya swag na kuringa, unajua Hemedi Suleiman na PHD ni watu wawili tofauti, nikiwa Hemedi sina mambo hayo kabisa, na nikiwa kama PHD hiyo is not me ni kuigiza tu..ila the only reason guys wana hate ni kwasababu wana deploma na nina PHD" amesema PHD.

Baada ya kumuuliza alipofikia kuhusu show yake aliyoiita "wife star search" maalumu kwa ajili ya kufanya shows sehem mbali mbali kutafuta mke hemedi alisema

"ile ilikua ni kwaajili ya kutafuta wife serious, ila baada ya kupokea simu kadhaa kutoka kwa mashekhe na kuniuliza "baba ako alifanya audition?" nikaona duuuh, wacha niachane nayo tu

Hemedi PHD kwa sasa ana ngoma yake inayofanya vizuri inayoitwa "going crazy" aliyoifanya chini ya producer Pancho ndani ya B Hits

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA