Mahakama
kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 Samsoni
Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia
ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma
mashtaka mbele ya jaji wa mahakama hiyo Samwel Karua, Mwendesha mashtaka
wa Serikali Rhoda Ngole alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni
21, 2010 kinyume cha kifungu cha 195 (16) kilichofanyiwa marekebisho
Mwaka 2002.
Ngole
aliiambia Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huo
majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku ambapo alifika nyumbani kwa baba yake
akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na baadaye kuidondosha sigala
hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
source DJ SEK
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA