source HYPERMAN HK
Na Imelda Mtema
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea
kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi
Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila
yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema
katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa
juzi Jumanne usiku kituoni hapo.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa
mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote
kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo
sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.
...Diamond na Jokate wakicheza.
“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya
mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na
alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo
hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe
nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana
na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana
aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper
ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia
wimbo wa Mawazo.
PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV,
Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake
kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny
ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na
Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona
kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu,
hata kama anafanya mambo yake ni kwa
siri.”Chanzo:www.globalpublishers.info
When it comes to fishing, some goes for fishing as an
ReplyDeleteentertainment activity and many depends upon fishing for their livelihood.
Never dawned on me that they might want to try it, so I was surprised
one day in the late-eighties when my son called and said they wanted to go fishing.
All the equipment is included in your deep sea fishing charter Cancun and the boat is so nice you will want to take advantage of the luxury fishing
afforded from the Querida del Mar.
Also visit my weblog: Visit posters website