Friday, January 25, 2013

MACHINGA KARIAKOO WAWAGEUZIA KIBAO MIGAMBO


machinga wadogo wadogo wa kariakoo jijini dar es salaam leo wameonesha hasira zao kwa migambo walio dai kuwa huwa wanawanyanyapaa na kuwapola malizao ambazo zinawasaidia kusukuma maisha yao.
 Mapema leo migambo walifika kariakoo na kuanza kuwakimbiza wamachinga na kuwakamata kama kawaida yao, kitendo hiki kimewakera machinga hao na kudai kuwa hili swala wamechoka nalo kwani huwa wanapolwa mali na pesa zao na migambo hao, waliamua kuwageuzia kibao machinga hao na kuwaambia leo sikukuu sio siku ya kazi iweje wao wawepo kazini,?
 wamachinga hao wakaanza kuwakimbiza migambo hao na kutaka kuwachapa ambapo polisi waligika kuwasaidia askali hao wajiji maarufu kama MIGAMBO,
 machinga waliamua kuwafikisha polisi migambo hao hata hivo hali haikuwa shwari kwani kulitawaliwa na vurugu za hapa na pale za wamachinga hao na kudai kuwa wamechoka kuonewa na migambo hao..
 hii ndio hali halisi iliojitokeza leo KARIAKOO

1 comment:

TOA MAONI YAKO HAPA