Wednesday, January 23, 2013

MAUJI YA KUSIKITISHA YATOKEA KATIKA CHUO CHA ST. JOHN'S DODOMA


Mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliekuwa anasoma nurse amekutwa amefariki katika njia iendayo chuoni hapo, taarifa za awali zinasema kuwa alikuwa anakuja kujisomea chuoni hapo mida ya usiku, inaonekana alikutana na watu wabaya wakati anakuja kujisomea na kumbaka maana nguo zake zilikutwa pembeni ya mwili wake, vilevile mwili wa marehemu huyo ulikuwa umeliwa  na  mnyama inasemekana kuwa ni fisi.



Hapa polisi wakiuchukua mwili wa marehemu huyo





                    Hapa polisi wanauweka mwili wa marehemu huyo kwenye gari, endelea kutufatilia kwa taarifa zaidi tutazidi wajulisheni.
JESHI la polisi mkoani Dodoma limeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa kinyama kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima na watu wasiojulikana.

Marehemu Lidya mwenye umri wa miaka 57 anadaiwa kuuawa siku ya jumapili hii majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa maeneo ya chuo hicho chenye wanafunzi 5500
akiwa anarejea nyumbani baada ya masomo ya jioni.

Ni simanzi,vilio,huzuni na majonzi katika vyunga vya chuo hiki kufuatia tukio hili la kusikitisha ambalo linadaiwa kuyaweka katika mashaka na wasiwasi mkubwa maisha ya wanafunzi hawa.

Licha ya kulitupia lawama jeshi la polisi baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa baada ya kufikwa na mkasa huo uliositisha safari ya maisha yake mwili wa marehemu Lidya uliharibiwa vibaya na mnyama asiyejulikana kwa kunyofolewa macho,masikio,pua,mguu na viuno vingine.

Prof.Gabriel Mwaluko ni makamu mkuu wa Chuo na Karimu Meshack ni afisa habari ambao kwa pamoja wanaelezea kilichorjiri.

Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo, Kamanda wa mkoa ACP David Misime anawataka wakazi wa mkoa huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.

Wakati huo huo Kamanda Misime anasema msako mkali umeanza wa kuwatia nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwa ajili ya hukumu.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA