Thursday, February 14, 2013

BREAKING NEWS: MSANII MAARUFU WA NIGERIA GOLDIE AFARIKI DUNIA USIKU WA VALENTINE DAY

 

 

Suzan Harvey aka Goldie

Ni taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page zake za facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria.
Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA