Wednesday, February 6, 2013

"JAPO KUNA WATU WANANIPONDA, LAKINI BIG BROTHER LAZIMA NITASHIRIKI"....T.ID

 
Nia ya Khalid Mohamed aka Top in Dar kutaka kushiriki shindano la Big Brother Africa mwaka huu iko pale pale licha ya kuwepo watu walionza kumkatisha tamaa.

Kupitia Facebook TID ameandika, “A Bad Company always corrupt a good character…I wont accept that, I WILL Be in a Big Brother Superstarz.”
Mwandishi wa ripoti hii  amempigia simu TID kutaka kupewa ufafanuzi wa alichokiandika ambapo amesema alimaanisha kuwa tangu Bongo5 imtaje kuwa miongoni mwa mastaa wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania katisha shindano hilo mwaka huu na watu wengi kumuunga mkono, kumetokea watu wachache wanaosema hatoweza.
TID amesema maneno hayo hayamkatishi tamaa na kwamba msimamo wake wa kuchukua fomu kujaribu bahati yake uko pale pale ambapo anatarajia kuichukua wiki hii.
“Hey bro! jst trust in urself go there n bliv t or not u gonna do smthng splendid,i adore u as wel as im ur fan so i bliv u wil do smthng so splendid and we as tanzanians we bliv in t…wsh ya ol da best, ” aliandika shabiki wake mmoja.
“As i have been buying ur albums,listening to your music,watching your videoz,come to ur show’z and many more……my positive support by VOTING alooooooooooooo……t for U@Tid Tid Topband,” aliandika mwingine.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA