Saturday, February 16, 2013

KATIKA PICHA: VALENTINE’S DAY ILIVYONOGA NDANI YA DAR LIVE

Linah Sanga akikamua.
Wapendanao wakijimwaya.
Kassim Mganga ‘Tajiri wa Mapenzi’ akiwanogesha wapendanao.
Kassim akipagawisha wapendanao sambamba na mwanadada mmoja.
Kiongozi wa Coast Modern Taarab, Omary Tego akiongoza kundi lake.
MC wa Dar Live, Pamela Daffa (kushoto) akiwapa zawadi wapendanao.
---
UMATI uliofurika ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burdani wa Dar Live huko Mbagala, jijini Dar es Salaam,  kusherehekea siku ya wapendanao ulinogeshwa na burudani mbalimbali pamoja na kujizolea zawadi kutoka kwa uongozi wa Dar Live ambapo Kundi la New Zanzibar Stars chini ya Ustaadh Issa Kamongo, lilianza kukamua na vibao vyake mbalimbali na kisha kundi hilo likalipisha Kundi la Coast Modern Taarab chini ya Omary Tego.
Baada ya makundi ya taarab kumaliza kufanya makamuzi na kuwaacha wapendanao wakifurahia mambo ya kukata nyonga, wasanii wa kizazi kipya nao walivamia jukwaa.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA