Monday, February 4, 2013

SOMA STORY BUIBUI AKIELEZEA CHANZO CHA AJALI ILIYOMPATA


100_4474
Msanii wa Bongo Flava Frank Kitende aka Buibui amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya weekend hii kugongwa na pikipiki na kupelekea kuvunjika mguu wake wa kushoto na wa kulia kuteguka.

Akiongea na 255 ya Clouds FM Buibui amesema tukio hilo limetoa usiku alipokuwa ametoka kufanya video ya wimbo wake na msichana aitwaye Lina J aliyeamua kumsindikiza baada usiku kuwa mnene.

Akiongea na 255 ya Clouds FM, Buibui amesema:
“Yule msichana nikamwambia kama vipi huu muda umeenda sana, mida ya saa saba saa nane, turudi tu home tukapumzike kwasababu kesho tena tunamalizia hii video,huku na huku tukaondoka, lakini katika wale vijana tuliokuwanao, mmoja simfahamu ila mwingine namfahamu, sasa huyo mshkaji alikua anamtaka huyo msichana, mi sijawahi kumtongoza, kwasababu namchukulia kama dada yangu naye ananichukulia kama kaka yake , na mimi sikupenda kwasababu yule sio malaya, nikaona bora nimrudishe yeye kwanza halafu na mi ndio nirudi kulala Kinondoni.

Buibui akiwa MuhimbiliBuibui akiwa Muhimbili
Kumshusha yule, sasa yule jamaa alikuwa kakaa mbele akawa kama amemaindi hivi, ‘kwanini Buibui kakubali tumrudishe huyu kwanza, kwanini asituache naye’, kwasababu alikuwa anafosi wanishushe mi kwanza halafu wao waendelee nae safari yao. Sasa yule dada akaniambia “Buibui, nipeleke mimi kwanza huwezi jua naweza nikafanyiwa kitu kibaya” kumrudisha akashuka wakawa wananirudisha mimi Kinondoni, basi kufika studio mi nikashuka lakini yule jamaa alikua kalewa akaanza kutoa shit huna lolote, nikashuka, nikawa natembea, sa wakati natembea kuna mshkaji akanambia mbona huyo jamaa ameshika jiwe kwa nia ya kukupiga, sa mi nikageuka kuangalia mshkaji gani huyu anaetaka kunipiga, wale wa bajaji kwasababu wananijua wakamuwahi , sa ile nageuka kushoto kwangu, narudi kuangalia kulia kwangu, nakutana na pikipiki na moto ikanigonga, lakini nilikua kwenye service road.”
100_4471

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA