Friday, February 22, 2013

UCHUKUWAJI WA PICHA ZA FILAMUUchukuaji wa picha za filamu ya World of Benefit unavyoendelea!
Na Claudi Zazou
Uchukuaji wa picha za fiamu ya World of Benefit unaendelea katika maeneo tofauti tofauti ndani ya jiji la Dare es Salaam ambapo wiki hii scene za hosptali zilipigwa.
Filamu hiyo imetokana na stori iliyoandikwa na Mwandishi mahiri wa Riwaya hapa nchini, Hamees Suba iliyokuwa ikijulikana kwa jina hilohilo la World of Benefit.
Filamu inashutiwa’ chini ya jopo la madairekta wakongwe watatu ambao ni Seles Mapunda (DoD),
Selemani Mkangara (Striker) na Director kutoka Bollywood, India, Samir Srivastava!
Mtayarishaji wa filamu hiyo, Hamees Suba ameeleza kwamba stori iliyomo ndani ya muvi hiyo inazungumzia mapenzi, nguvu ya pesa na utoto wa mjini.
Upande wa kamera, taa na sauti umesimamiwa na ‘cruew’ kutoka Bollywood (India) chini ya kampuni ya Pilipili Entertainment ikiongozwa na Bwana Ajay.
Mastaa walioshiriki katika filamu hiyo ni mshindi wa tuzo ya Ziff Rose Donatus Ndauka, Hemed Suleiman Phd, Awadh Saleh, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Thecla Mjata ‘Mama Mjata’ na mwanamuziki Ali Timbulo.
Washiriki wengine ni Peter, Miriam Bashiri, Tutti Rahman, Latipher Mkuu, Natalia Mossi na wengineo.
Meneja Mzalishaji Mkuu wa filamu hiyo, McDenis Mgatha, amesema kuwa kila msanii aliyeshirikishwa katika filamu hiyo ametokana na vigezo vilivyohitajika ndani ya stori.

DSC00636.JPG
DSC00637.JPG
DSC00658.JPG
DSC00646.JPG 
DSC00659.JPG
DSC00661.JPG  
DSC00664.JPG
DSC00684.JPG
DSC00696.JPG

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA