Saturday, March 16, 2013

MVUTA SIGARA APEWA HUKUMU YA MIAKA 35 JIJINI MBEYA BAADA YA SIGARA KUSABABISHA MAUAJI YA WATU 7




Mahakama kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 Samsoni Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia ndugu wa familia moja wapatao saba.



Akisoma mashtaka mbele ya jaji wa mahakama hiyo Samwel Karua, Mwendesha mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha 195 (16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.



Ngole aliiambia Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huo majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku ambapo alifika nyumbani kwa baba yake akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na baadaye kuidondosha sigala hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
source DJ SEK

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA