Tuesday, January 29, 2013

HATIMAYE LULU YUKO HURU URAIANI....TAZAMA PICHA NA HABARI HAPA

 Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo.
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
 --------------------------------
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA