Galatasaray imemsajili aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba
kutoka kwa klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki katika ligi kuu ya
Premier nchini Uchina.
Galatasaray
inayocheza ligi kuu nchini Uturuki, imethibitisha kuwa Drogba amesaini
mkataba wa miezoi kumi na minane na klabu hiyo.
Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa
yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika
mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya
uhusiano bora inayomuakilisha mchezaji huyo Sports PR Company na
kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa Twitter, Drogba alisema
anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe la klabu binga
barani ulaya kwa mara nyingine.
Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.
''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi kupuuza'' Alisema Drogba
Source: BBC
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA