|
Ni mchaka mchaka ulioendana na nyimbo za hisia |
|
Msafara hapa unaelekea maeneo ya Bungeni |
|
Kila walipopita walikuwa wakishindikizwa na polisi kuhakikisha amani inatawala |
|
Gari la maji ya kuwasha lilikuwepo lakini wanafunzi hao hawakutishika na kitu chochote kile kutoka kwa Polisi |
|
Wanafunzi walifika mpaka Nyerere Square waliimba nyimbo mbalimbali mahala hapo |
|
Baada ya kutembea mji mzima na mabango yao na kuhakikisha kiu yao imekwisha basi waliamua kurudi chuoni |
|
Gari la washa washa nalo lilikuwepo lakini watu walikuwa na jaziba zao vilevile mwanzo mwisho |
|
Barabara zilikuwa zimetawaliwa na wanafunzi kwa kiasi kikubwa, mpaka kusababisha magari kutopita |
|
Hapa
ilibidi nipande gari la polisi ili niweze kuchukua picha vizuri, sio
siri polisi wenyewe walikuwa wamechoka kwa kutembezwa mji mzima baada
kuchat nao kwenye gari ilo |
|
Hapa
ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia
maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration. |
Safari ya maandamano ya amani ikawa
imeishia chuoni hapo baada ya kuona kuwa ujumbe wao umefika. Wanafunzi
wa chuo wamechoshwa na matendo mabaya ambayo wanafanyiwa ikiwa ni pamoja
na kubakwa, kulawitiwa, kuibiwa vitu vyao kama Laptop na vitu vingine.
Wameonesha umoja wao kwa sababu ya kuchoshwa na mambo hayo, ambapo leo
asubuhi kuna wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop. Hivyo wakaamua
kujikusanya asubuhi hiyo hiyo mida ya saa kumi na mbili alfajili na
kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye walimpiga na baadae
kuchukuliwa na polisi.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA