Nimeshuhudia leo maeneo ya TAZARA teja mmoja kapigwa na watoto wa mitaani nusu kuuwawa, chanzo ni kuwa jana kunawizi umetokea maeneo ya BAKHRESA na kwakua baadhi ya watoto wa mitaani wanalala pale hivo moja kwa moja wakahisiwa kuwa wao ndio wameiba, swala hili watoto hawa hawajalikubali kabisa na kuamua kuzunguka vituo vya daladala vya jirani na kusaka wezi hao, kwakuanzia tu hawa watoto wa mitaani pale pale tazara wamempiga na kumjeruhi sana teja mmoja wanae muhisi uwenda kahusika na wizi huo, wamempiga vibaya sana ameharibika sana na kuvuja damu nyingi hadi kupoteza fahamu, teja huyo kawaishwa hospitali ya TEMEKE,,, Blog yangu bado inaendelea kuchunguza hali ya teja huyo mahututi na kutaka kujua kwanini watoto hao wameamua kufanya unyama huo,,,,,,
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA