Suzan Harvey aka Goldie
Ni
taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page zake za
facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti
kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI
muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo
bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
Mmoja
wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter
ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa
february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria.
Taarifa
nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana
kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya
CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya
kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya
TV.
Prezzo
alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja
ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na
Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na
kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA