Tuesday, February 12, 2013

MATUMAINI ANAHITAJI MSAADA KUTOKA KWA WATANZANIA

Stori: Gladness Mallya
LICHA ya afya ya msanii wa vichekesho nchini, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ kuonekana kuendelea vyema na kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Amana jijini Dar, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji nchini, Michael Sangu ‘Mike’ amewataka wadau kumsaidika ili afanyiwe uchunguzi zaidi.


Mike aliyasema hayo hivi karibuni alipoongea na Tollywood Newz na kubainisha kuwa Matumaini anatakiwa afanywe uchunguzi wa figo na ini ili aweze kupona kisawasasawa
.
“Ingekuwa vyema kama tungejitolea kumsaidia apate vipimo kwenye hospitali kubwa, kwani amerudishwa nyumbani lakini siyo mtu mwenye hali ya kuridhisha

SOURCE  GLOBAL

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA