Saturday, February 2, 2013

CANDY: NAPENDA KUFANYA NINACHO JISIKIA..

Nikiwa bado mgeni kwenye muziki wa bongo fleva bado nahitaji kujifunza mengi na kujua mengi zaidi kutoka kwa wakongwe wa bongo fleva,
kwasasa nina nyimbo mbili ambazo tayari nimeziachia radioni na pia waweza kuzisikiliza kwenye blog hii na kutazama video zake hapa,pamoja na hizo nyimbo mbili ambazo tayari nimetoa bado nina nyimbo nyingi saana nilizo andika na baadhi zimesharecodiwa ila bado naumiza kichwa saana kutafuta merod na mashairi mazuri ili nami siku moja nije kuvuma kama wenzangu walionitangulia

Ninaposema napenda kufanya ninacho jisikia namaanisha kuwa napenda kuwa mimi kama mimi na watu wanielewe kuwa ni mimi, sipendi kuiga yale yanayo weza kunipotosha na kuniweka pabaya,  muda mwingi naupoteza kufanya mambo yangu binafsi ninayo hisi yataniletea mafanikio baadae pia nashukuru mungu tangu nimekuwa na hii blog naona mambo yamebadilika sio kama mwanzo kwani inanisaidia kujitangaza na kupata fans weengi na watu wengi wamekuwa wakizipata nyimbo zangu kiurahisi saana hii ni kutokana na jinsi ninavo jitahidi kuzisambaza kwa njia ya mtandao wa kijamii,

Wasanii wa bongo inabidi ifike kipindi tujiullize sisi ni nani na kipi tunatakiwa kuifanyia nchi yetu ili ishine kama nchi zingine zinavoshine na muziki wao wa nyumbani. hata katika uandaaji wa nyimbo lazima ujiulize hii nyimbo yaweza vuka mipaka na ikapendwa au itaishia hapa hapa tu?,,
        Muziki ni sehemu ya maisha yangu nilioipa nafasi kubwa saana na naamini utanifikisha pale ninapo hitaji kufika na pengine watu wasioijua tanzania wakaijua kupitia mimi,..........
              Hayo ni machache nilioamua kuongea na shabiki wangu weekend hii,
                                           NAWAPENDA
                   ,,,CANDY CALFONIA

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA