Saturday, February 9, 2013

HOUSE BOY KAPEWA MATESO NA BOSI WAKE MPAKA KUFA

Inauma sana! Imeelezwa kuwa msoto wa mateso aliyopitia kijana Isaack Banda, raia wa Malawi ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani na bustani (house and shamba boy), aliyedaiwa kuchomwa moto na mwajiri wake hadi kusababisha kifo chake, yalikuwa
makuu,  limenyetishiwa



 

Picha ya kijana Isaack Banda, raia wa Malawi ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani na bustani wakati wa uhai wake


Ndugu na jamaa wakiwa katika mazishi
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea wiki iliyopita nyumbani kwa mwajiri wake huyo maeneo ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Ilifahamika kuwa chanzo cha kukutwa na mateso hayo ya kutisha hadi kifo, mwajiri wake alimtuhumu kumwibia mali zenye thamani ya dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya Sh. milioni 80), zilizokuwa ndani ya nyumba aliyokuwa akilinda na kuitunza iliyopo Kinondoni, Dar.


Banda akiwa hospitali kabla hajafariki dunia
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu waliozungumza , kijana huyo alikuwa na takribani miaka miwili akifanya kazi kwa mwanamke huyo ambaye pia ana uraia wa Marekani.
Kuna madai kuwa baada ya kumtuhumu kwa wizi, kijana huyo alifungwa kamba ili asifurukute, akapokea kikombe cha mateso kabla ya kuchomwa moto na kubaki na majeraha ambayo yalisababisha kifo chake akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ndugu hao walidai kuwa huku jamaa akijitetea kwa namna zote kuwa hajui chochote juu ya upotevu mali hizo, watesaji hawakumsikiliza pamoja na kwamba aliwaeleza kuwa ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na ndugu wengine na mshirika wa kibiashara wa mwajiri huyo, mwenye asili ya Asia, ambao nao walipaswa kubanwa.
Walidai katika hali ya kusikitisha zaidi, watesaji hawakutaka kumsikiliza hadi walipoona ana hali mbaya ndipo wakamtelekeza kabla ya kuchukuliwa na wasamaria wema kupelekwa hospitali alikokutwa na umauti.
Juzi Jumatatu, Tulifika katika Makaburi ya Mwananyamala Kwa Kopa, Dar na ku-shuhudia umati wa waombolezaji wakiwa katika mazishi ya jamaa huyo huku kila kona makaburini hapo ikitawaliwa na majonzi.
“Kuna vifo lakini hiki cha Banda kinauma zaidi. Jamaa aliteseka sana,” alisema mmoja wa waombolezaji hao.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo linamshikilia mwanamke huyo ili kusaidia uchunguzi wa shauri hilo

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA