Written By Tryphone Nyahinga on Tuesday, February 19, 2013 | 10:24 PM
UPDATES: Blade runner na nyota wa paralympic Oscar Pistorius, leo hii
amejikuta akimwaga machozi baada ya kuanza kutajwa kosa lake la kwanza
la mauji katika mahakama ya hakimu , Pretoria leo hii asubuhi.
hakukubaliana na shtaka kuwa kamuua mpenzi wake ambae alikua ni model
wa FHM, Reeva Steenkamp, katika masaa ya mwanzo ya siku ya valentine
waendesha mashtaka waliiambia mahakama hiyo kuwa, wanaweza kubishana
kuwa yale yalikua ni mauaji yaliyopangwa kabla, na mauaji serious zaidi
yenye kuchukua adhabu ya kufungwa maisha jela
kuondokana na hisia, pistorius alifarijiwa na baba yake, kaka zake na
dada zake baada ya kuskika sauti ya kilio cha kwikwi kutoka kwake ndani
ya chumba cha mahakama kilichokua kimejaa watu.
kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya kuibuka kwa picha ya silaha
inayoaminika kuwa ni 9amm pistol, inayosemekana kutumika katika mauaji
hayo. ilionekana katika mfuko wa plastic ukiwa umebebwa na polisi
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA