Written By Tryphone Nyahinga on Tuesday, February 19, 2013 | 3:02 PM
NIMEKUELEWA MBUNGE WANGU MNYIKA
Nimeisoma vizuri taarifa ya bwana Mnyika na nimeielewa. Nimeona sababu za msingi kwa nini hakumaliza shule na majibu juu ya hoja ambayo aliisimamisha bwana Nape Nnauye.
Ni jambo zuri ambalo amelifanya maana tumefunguka na kujua ukweli. Lakini naomba radhi kama sikueleweka vizuri. Nilichofanya mie ni kumuita ukumbini ili atutoe wasiwasi hasa mimi kama nilivyojielewa kuwa nilikuwa naye chuoni na ninaheshimu sana uwezo wake wa ufahamu.
Mwisho nimuhakikishie, ni jukumu la CCM kuhakikisha kuwa maji yanapatikana Jimboni Ubungo na tutayaleta. Kubwa zaidi akumbuke ilani yetu ni ya miaka mitano na maji yatafika pale kabla ya 2015. La msingi aendelee kuisukuma serikali na kumkumbusha waziri maghembe juu ya utekelezaji wa ya maneno yake mazuri na sio mbwembwe za kufurahisha baraza.
Mwisho, nikupongeze mnyika kwa kuja hadharani na kutoa wingu. Ni imani bwana Nape na wasomaji wengine tumekuelewa.
Shukrani. Hatuchafuani, tunasaidia kuwekana sawa . Huu ndiyo uwazi kwa vitendo.hongera muhes

No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA