TAARIFA
kutoka kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zilizotumwa katika
mitandao ya Kijamii na Bi Hellen Kijo bisimba mchana huu zinapasha kuwa
kuzuka vurugu na kusababisha majeruhi huko Wilayani Chato.
Tumepokea
taarifa za masikitiko kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato
kuhusu uchinjaji wa nyama unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.
Chanzo cha Habari hizi kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama.
Baaadhi
ya Wakristo waliamua kuanzisha bucha ya ili wachinje na kununua hapo
ili wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya
Kiislamu kwa vile uchinjaji kwa Waislam ni ibada.
Baada
ya kufungua Bucha hiyo leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa
kuwa waislam walifika kutaka kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao
walifika na walitaka wamchukue mwenye bucha hiyi.
Suala hili likazua tafrani na pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na kuna watu wameumizwa.
Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha ufungwaji wa bucha nazo zimeharibiwa.
Baada
ya kupokea taarifa hii tumewatuma waangalizi wetu wa haki za binadamu
kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama watakavyoweza.
Tunahabari
kuwa kikosi cha kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo
tunaloliona kwa haraka ni kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa
kuyatazama masuala kama haya na kuyawekea msimamo na maelekezo kabla
vurugu kama hizi kutokea.
Pili
tunaona kuwa hali ya kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo
ambalo ni hatari sana kwa usalama na amani hapa nchini.Wakati
tunasubiri taarifa zaidi tunapenda kutoa angalizo kwa viongozi wetu
maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari ameshafika katika eneo la tukio.
Masuala
kama haya yatazamwe kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia
kwa kuzingatia haki za binadamu na hususani haki za kiraia na
kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa ibada na kila mtu asiingiliwe katika
haki hizi.
Lakini
pia njia za utatuzi wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali
pawe na nafasi yamaongezi ya kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro.
Tutaweza kutoa taarifa zaidi tutakapopokea taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya mgogoro au vurugu hizi
Chanzo Juma Mtanda Blog
Candy we thank you for you information, we pray thus the issue should be solved peacefully and our learders should find a good method of solving this and stop this religious conflict. Regars, Frans
ReplyDeletetanx guyz
ReplyDelete