Tuesday, January 22, 2013

BOB JUNIOR.... HATIMAYE NIMEKUWA BABA AHSANTE MUNGU

Mkali wa muziki wa kizazi kipya BOB JUNIOR hivi karibuni amepata mtoto, BOB junior ni msanii anae jituma sana na kufanya muziki wake kwa malengo na kuipenda kazi yake, naweza sema ni kati ya wanamuziki wanaoshine sana kwa sasa na daima anasisitiza UTANASHATI, mkali huyu kashafanya vizuri sana kwenye nyimbo zake kama OYOYO, NICHUMU na zingine pia ameweza kuisimamisha studio yake kwa kasi sana kutokana na kazi nzuri,naweza sema amekuwa ni prooducer mkali na anae wajali na kuwasikiliza wasanii wake, wengi wanafurah jinsi anavopenda kucheka hii inaashiria ni upendo na amani wakati wote,
sasa amekuwa baba, ,,,,"' nitatulia na kufanya yote ambayo baba anatakiwa kutimiza kwenye familia, maisha yangu yamebadilika sana najiona kama mungu kanipendelea kunipa mtoto wakati muafaka nikiwa na nguvu za ujana na akili, nitaendelea kupigana na maisha na kuhakikisha mwanangu anakuwa katika malezi bora ya ya kidini vile vile bado nitaendelea kuisimamisha studio yangu ya SHAROBARO REC na kuzidi kutoa kazi nzuri zaidi"' BOB JUNIOR

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA