Monday, January 28, 2013

HALI YA MTWARA SASA NI SHWARI.....

UTULIVU WAREJEA MTWARA BAADA A WANAJESHI WA JWTZ KUINGILIA KATI , ZAIDI YA WATU 40 WAKAMATWA


Hali ya  utulivu  inadaiwa  kurejea katika wilaya ya Masasi  mkoani Mtwara baada ya   vikosi  vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na  polisi  kuungana  kuweka ulinzi huku  watu  zaidi ya 40  wakikamatwa  kuhusika na matukio  ya vurugu za jana.

Taarifa zinasema   kuwa kutokana na vurugu  hizo  waziri mkuu Mizengo Pinda na  waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku  wa kuamkia leo walikuwapo Mtwara  wakiendelea na vikao  vya  kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.

Pia inadaiwa  mida ya asubuhi  leo  polisi  walilazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  vijana ambao  walikuwa  wamefunga barabara na  kuwatoza ushuru  batili  wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.

Mbali ya tukio  hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara  kwa siku ya leo shughuli  zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara zimesimamishwa kwa  muda  ili  kukwepa vurugu kama za jana  japo shughuli za ibada  zimeendelea kwa  utulivu  zaidi.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA