Saturday, February 16, 2013

AZAM YAANZA VYEMA KOMBE LA SHIRIKISHO YAICHAPA AL-NASRI 3-1


Kiungo wa timu ya Azam FC, Bolou Kipre (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Abdallmelik Sebit, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Azam, imeibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mabao ya Azam yamefungwa na Abdi Kassim, katika kipindi cha kwanza, na mabao 2 yamefungwa na Kipre Tchetche katika kipindi cha pili.
 Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la pili la timu yao lililofungwa na Kipre Tchetche (katikati) wakati ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya El -Nasir ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Kipre Tchetche (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Al-Nasri.
 Jabir Aziz akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa El Nasir FC ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umomy akiwatoka walinzi wa timu ya El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Jacob Osuru na Abdallmelik Sebit katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha el Nasir ya Sudan ya Kusini
 Kikosi cha Azam FC
Mashabiki wa Azam, wakishangilia

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA