Friday, February 22, 2013

GARI LA KANUMBA LAMSHINDA DK. CHENI...AAMUA KULIRUDISHA KWA WENYEWE

GARI la aliyekuwa staa wa filamu Bongo Steven Kanumba aina ya Toyota Land Cruiser V 8, imeelezwa linapigwa bei na limeshindikana kuuzika kwa sababu ya bei kuwa kubwa ukilinganisha na hali ya mkoko wenyewe ilivyo kwa sasa.
  
Marehemu Steven Kanumba akiwa jirani na gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V 8 enzi za uhai wake.
Habari za ndani kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba, mteja aliyekuwa akitegemewa zaidi ni msanii maarufu nchini, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ambaye baada ya kutajiwa bei alipewa kwa ajili ya kulifanyia majaribio.

CHANZO KINATIRIRIKA
Kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini chanzo hicho kilitiririka kuwa, si kweli kuwa Dk. Cheni alipewa lile gari ili alitumie kwa muda kufanya vifaa visiharibike bali alikuwa akilijaribu.
“Unajua ndugu yangu lile gari wenyewe (familia ya Kanumba) wanaliuza milioni 40, Cheni amelikagua sana akagundua lina matatizo mengi ndiyo maana akawaambia atoe milioni 25 wamekataa na sasa limemshinda na ameshalirudisha,” kilipasha chanzo.
 
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’.
MATATIZO YENYEWE
Kikiendelea kutambaa na mistari, chanzo hicho kilitaja baadhi ya matatizo ya gari hilo, kikasema: “Kwanza namba zake za usajili ni za zamani ni T 750 AER, gia boksi ina matatizo ambayo yamesababishwa na gari hilo kutumika likiwa kwenye four wheel ndiyo maana gia boksi imepata matatizo.
“Halina motor vehicle,  steeling power mbovu, halina road licence na mbaya zaidi kwa namna lilivyo kwa mizunguko ya kawaida mjini, kwa siku linatumia mafuta ya laki moja.
Vyote hivi Dk. Cheni aliviorodhesha na kwenda kuwaeleza ili wapunguze bei lakini wamegoma, wanataka milioni 40 wakati Cheni ameng’ang’ania kuwa anataka kutoa 25 (milioni).”

DK. CHENI KIZIMBANI
Baada ya kupata maelezo haya kutoka kwa chanzo, Ijumaa lilimvutia waya Dk. Cheni na kumuuliza juu ya madai hayo, alisikiliza kwa makini sana maelezo yote hadi mwisho, alipotakiwa kujibu, akakata simu kisha akazima kabisa.

SOURCE: GPL

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA