Friday, February 22, 2013

HII NDO HISTORIA YA PRODYUZA P FUNK ALIPOTOKA NA ALIPO SASA
KUTOKANA na kuwa na upungufu wa maprodyuza kwa miaka ya 1990 hali ilisababisha kunishawishi kuwa prodyuza ili kuutambulisha muziki wa Tanzania katika mataifa mbalimbali nje ya fani ya kutengeneza muziki, ni muimbaji mzuri hususani wa Hip Hop hayo ni maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na prodyuza Paul Matthysse anayejulikana kwa jina la P Funk Majani alipokutana na Spoti Majira wikii hii

Alianza kupenda kufanya muziki mwaka 1992 huku akiwa ameunda kikundi cha muziki kilichokuwa kinajulikana kwa jina la 'Street Wisdom' kwa kipindi hiko alitumia muda wake mwingi kufanya muziki kwani ndio kitu alichokuwa akikipenda

Alikuwa anapenda kuimba muziki wa Hip Hop kwa kipindi hiko cha miaka ya 90, ingawa kwa sasa ni produza anamiliki studio ya Bongo Records, huku akibainisha kuwa studio hiyo imewatoa mastaa wengi akiwemo msanii Juma Nature na wengine wengi

Kutokana na hali ya kupenda kufanya Hip Hop alijikuta analazimika kubadili fani na kuingia katika prodyuza huku akiwa na ndoto lukuki za kutengeneza muziki wenye ubora wa kimataifa na kuutangaza muziki kwenye ngazi ya kimataifa

Kwa kipindi chote hicho aliweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa kuutambulisha muziki hapa nyumbani na kuleta changamoto tofauti hali iliyosababisha mapokeo ya muziki huo kuwa mazuri na mashabiki kuukubali muziki wa bongo fleva

Alianza safari ya kuwa produza mwaka 1997 wakati ambao watu wengi hawaelewi muziki na kulikuwa na dhana tofauti tofauti huku baadhi ya watu wakidai anayefanya muziki ni muhuni wengine wakidai muziki ni wa watu furani kwenye jamii

Aliweza kung'araa zaidi alipokuwa Produza kwa kukuza vipaji vya wasanii wengi na kuufanya muziki wa Tanzania uweze kujulikana ndani na nje ya nchi huku akibainisha kwamba albamu ya Feruz Mrisho iliyobeba jina la Starehe ndiyo iliyoongoza kwa mauzo kwa kufikia nakala 500,000 katika wasanii wote waliokuwa kwenye lebo yake

Hakuwa nyuma kwa kuwa na mikakati ya kuufanya muziki utambulike kwani alikuwa ni mtu ambaye anaweza kuandaa 'concert' za uzinduzi wa albamu mbalimbali za wasanii waliokuwa chini ya lebo yake na aliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani mpaka sasa hakuna msanii aliyeweza kuipita rekodi ya Juma Nature wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya Ugali alipoweza kujaza mashabiki katika ukumbi wa Diamond

Mikakati hiyo bado anaendelea nayo kwa kuwaomba wadau wa muziki wajitokeze kudhamini shoo hizo kwani wananchi na mashabiki bado wanahitaji kuona wasanii wao wanafanya uzinduzi wa aina hiyo, hali hiyo itasababisha kuepusha  wasanii kufanya uzinduzi wa single zao katika club huku idadi ya mashabiki wakizidi kupungua siku hadi siku

Kwa sababu ya kupenda kuimba muziki wa Hip Hop mwaka jana prodyuza Pfunk aliamua kufufua kundi la muziki linaloundwa na watayarishaji wakali wa muziki wa bongo fleva akiwemo John Mahundi, Lamar huku wakiwa wameachia single yao inayojulikana kwa jina la 'No Name'

Siku za mapumziko anapenda kwenda ufukweni kupunga upepo huku akiamini kuwa mawazo mapya na ubunifu mwingine anaupata akiwa katika maeneo hayo ya ufukwe

Anapenda sana rangi nyekundu na huchagua rangi nyekundu kwenye mavazi yake huku akiamini kuwa rangi hiyo humaanisha hatari ingawa si hatari kwenye maisha yeake

SOURCE: BONGOCLAN BLOG

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA