Thursday, February 28, 2013

SAKATA LA "BINTI KIZIWI " KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA


SIKU chache baada ya mrembo wa video ya wimbo wa Binti Kiziwi wa Ally Mohammed ‘Z.  Anto’, Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kunaswa na madawa ya kulevya nchini China, Jacqueline Patrick ‘Jack’ ambaye ni modo kiwango Bongo, amesema anajua kila kitu kuhusu tukio la kukamatwa kwake, Amani linakuhabarisha.

Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum juzi, jijini Dar es Salaam kuhusu uvumi ulioenea kwamba yeye ndiye aliyemchoma Binti Kiziwi kwa polisi na kusababisha kudakwa kwake, alisema tuhuma hizo si za kweli bali ni mbinu za watu wanaotaka kumchafua.“Ngoja nikuambie ukweli, siku Binti Kiziwi anakamatwa mimi nilikuwepo uwanja wa ndege na niliona kila kitu. Unajua mwanzo alianza kulalamikia tumbo kumsumbua ghafla, akachukuliwa na kupelekwa kupewa huduma ya kwanza.

“Akiwa huko kwenye matibabu alipigwa ultrasound ndipo alipogundulika kuwa kumbe alikuwa na vitu tumboni.


Katika hali kama hiyo unadhani ni mjinga gani anaweza kujitokeza na kudai huyo ni ndugu yake?”


“Mimi sijui chochote lakini nilichojua yule ni Binti Kiziwi na ni Mtanzania mwenzangu, tena staa kama mimi kwa hiyo sikuwa na sababu ya kumchoma ila ilivyogundulika hivyo nisingeweza kujitokeza maana na mimi pia ningetakiwa kuisaidia polisi kwenye uchunguzi.


“Kubwa kuliko yote, yeye ni ndugu yangu kabisa. Mama yake na mama yangu ni ndugu, nisingeweza kumchoma.”“Jambo la muhimu nililoamua kufanya ilikuwa ni kutoa taarifa kwa ndugu zake wengine ili waweze kumsaidia.


 Nilifanya hivyo kwa wakati. Siku zote nimekuwa karibu naye, hata nikienda China huwa nakwenda kumtembelea gerezani,” alisema Jack.
 
source MPEKUZI

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA