Friday, February 1, 2013

SUMALEE ASHINDWA KUMZIKA BABA YAKE

.


Miezi 8 toka mama yake mzazi afariki dunia, msanii wa bongofleva Sumalee amepata pigo jingine baada ya baba yake mzazi kufariki january 31 2013.
Taarifa zilizoifikia dj-sek.blogspot.com ni kwamba baba yake alifariki jana jioni wakati bado Sumalee yuko Uingereza kwa shughuli za kimuziki.

Namkariri akisema “mama yangu amekufa kwenye mikono yangu, yuko kwenye mapaja yangu na mikononi nilikua namsomea dua tu”
Kulikua kuna taarifa kwamba Sumalee kapata matatizo ya hati yake ya kusafiria huko Uingereza hivyo itakua ngumu kuja Tanzania msibani lakini taarifa nilizonazo kutoka kwa mtu wa karibu ni kwamba hajapata tatizo lolote kama wengi wanavyodhani, kilichotokea ni kwamba alitaka kuongeza miezi sita ya kuendelea kukaa Uingereza hivyo ikabidi Passport aiache ubalozini ambapo ghafla ndio akapata msiba hivyo itabidi asafiri kwa kutumia documents.
Mtu huyu wa karibu wa Sumalee ameiambia  dj-sek.blogspot.com kwamba baba mzazi wa Sumalee anazikwa leo february 1 2013 na Sumalee wamejaribu kuwasiliana nae hapatikani kwenye simu hivyo hakuna uhakika kama yuko kwenye ndege kuja Tanzania ama la.
dj-sek.blogspot.com inatoa pole kwa Sumalee, familia na ndugu kwa msiba huu

Souce: Millard Ayo

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA