Monday, February 11, 2013

TAARIFA YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU KUHUSU KINACHOENDELA GEITA, VURUGU ZA KIDINI


[Image: 4.jpg]
 
TAARIFA kutoka kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zilizotumwa katika mitandao ya Kijamii na Bi Hellen Kijo bisimba mchana huu zinapasha kuwa kuzuka vurugu na kusababisha majeruhi huko Wilayani Chato.
 
 
 
Tumepokea taarifa za masikitiko kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato kuhusu uchinjaji wa nyama unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.
 
 
 
Chanzo cha Habari hizi kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama.
Baaadhi ya Wakristo waliamua kuanzisha bucha ya ili wachinje na kununua hapo ili wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya Kiislamu kwa vile uchinjaji kwa Waislam ni ibada.
 
 
 
Baada ya kufungua Bucha hiyo leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa kuwa waislam walifika kutaka kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao walifika na walitaka wamchukue mwenye bucha hiyi.
 
 
 
Suala hili likazua tafrani na pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na kuna watu wameumizwa.
Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha ufungwaji wa bucha nazo zimeharibiwa. 
Baada ya kupokea taarifa hii tumewatuma waangalizi wetu wa haki za binadamu kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama watakavyoweza.
 
 
 
Tunahabari kuwa kikosi cha kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo tunaloliona kwa haraka ni kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa kuyatazama masuala kama haya na kuyawekea msimamo na maelekezo kabla vurugu kama hizi kutokea.
 
 
 
Pili tunaona kuwa hali ya kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama na amani hapa nchini.Wakati tunasubiri taarifa zaidi tunapenda kutoa angalizo kwa viongozi wetu maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari ameshafika katika eneo la tukio.
 
 
 
Masuala kama haya yatazamwe kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia haki za binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa ibada na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.
 
 
 
Lakini pia njia za utatuzi wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi yamaongezi ya kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro. 
Tutaweza kutoa taarifa zaidi tutakapopokea taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya mgogoro au vurugu hizi
Chanzo Juma Mtanda Blog

2 comments:

  1. Candy we thank you for you information, we pray thus the issue should be solved peacefully and our learders should find a good method of solving this and stop this religious conflict. Regars, Frans

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO HAPA