Sunday, February 10, 2013

TASWIRA MBALIMBALI ZA MAANDAMANO NA MKUTANO WA CHADEMA JIJINI DAR LEO


Written By Tryphone Nyahinga on Sunday, February 10, 2013 | 6:17 PM
Viongozi wa Chadema wakiwa katika mshikamano mkubwa, wakiandamana kupinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na Spika na Naibu wake dhidi ya wabunge wa Upinzani.
Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza kuunga mkono maandamano yaliyoandaliwa na Chadema kupinga uonevu wanaofanyiwa wabunge wa Upinzani Bungeni.
Viongozi wa Chadema wakiwa meza kuu kutoka kushoto Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa, Mwenyekiti Mhe. Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe. Tundu Lissu akiongea kwenye mkutano uliofanyika Viwanja vya Mwembeyanga.
Mhe. Mnyika akiongea katika mkutano.
Kamanda Lema naye akimwaga cheche jukwaani.
Maandamano yakiendelea kuelekea Mwembeyanga.
PICHA ZOTE NA CHADEMA BLOG

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA