Friday, February 8, 2013

WAREMBO WA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 KUANZA ZIARA WIKI IJAYOs


Baadhi ya warembo wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika pozi.
WAREMBO wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani. Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha Makumbusho, Makumbusho ya Taifa, Pugu Sekondari, maeneo mengine ni ufukwe wa Kigamboni, soko la kimataifa la Magogoni, Uwanja wa Taifa na sehemu nyingine nyingi.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA