Thursday, March 7, 2013

ABSALOM KIBANDA AKIWA HOSPITALINI MUHIMBILI BAADA YA KUVAMIWA NA KUUMIZWA VIBAYA,


Kibanda akiwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).
Baadhi ya majeraha aliyoyapata Kibanda.
Kibanda akiendelea kupata matibabu ICU.
Waziri wa Afya, Dk. Hussein Mwinyi, akimjulia hali Absalom Kibanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Habari Corporation, Hussein Bashe, akimpa pole Kibanda.
Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (kulia) akimpa pole, Afisa Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Habari Corporation, Hussein Bashe.
Wanahabari wakimjulia hali Kibanda pamoja na kupata machache kutoka kwake.Picha na Richard Bukos na Haruni Sanchawa-GPL
---
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Corporation, Absalom Kibanda, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiojulikana wakati akivuka geti kuingia nyumbani kwake na gari yake aina ya Nissan.

Wavamizi hao walivunja kioo cha gari lake na kumchomoa ambapo walimpiga mapanga na kumjeruhi vibaya jicho la kushoto. Baada ya kufanyiwa unyama huo Kibanda alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.
SOURCE : DJ SEK

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA