Friday, March 1, 2013

GLOBAL PUBLISHERS, BONGO MOVIE ZATOANA JASHO NETIBOLI

Zainab Nassoro wa Global Publishers akipeleka mashambulizi mbele.
Mshambuliaji wa Bongo Movie, Monalisa, akiwa na mpira bila kuona wa kumpasia baada ya kubanwa na wachezaji wa Global.
Wachezaji wa Bongo Movie, Monalisa na Ummy (kulia) wakipelekwa puta.
Beki wa Global, Bahati Haule (kulia) akimtuliza Monalisa aliyekuwa akitaka kulia baada ya kuzidiwa.
Shabiki wa Bongo Movie, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, akishangilia baada ya timu yake kupata goli.
Ummy akigangwa baada ya msuli kumbana.
Monalisa akipashwa.
Msahabiki wa Bongo Movie wakishangilia baada ya timu yao kuibuka na ushindi.
Meneja wa timu za Global, Elvan Stambuli akionesha jinsi ya kupachika mabao kiufundi.
TIMU ya netiboli ya Global Publishers jana ilimenyana na timu ya Bongo Movie katika mchezo mkali uliofanyika Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.  Katika mchezo huo Bongo Movie iliibuka na ushindi wa mabao 25 – 15.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA