Saturday, January 19, 2013

KILIO CHANGU

Napenda sana watoto na napenda kucheza na watoto tangu nilipokuwa mtoto hadi sasa, watoto ndio taifa bora la kesho endapo watalelewa kwa misingi mizuri na maadili mema, kunabaadhi ya watu wanajaribu kuwajali sana watoto wao hata kama wanakipato kidogo ila kuna baadhi ya familia hasa hasa upande wa kina baba wanavipato vizuri ila hawawajali watoto wao, naichukia sana hii tabia na ingekuwa amri yangu ningeweza kuwashtaki hawa watu sababu endapo utamjengea mazingira ya ukatili mwanao uliemzaa unakuwa unamuharibu kisaikolojia baadae wengi wao wakikua nao wanakuwa na tabia hizo za ukatili, endapo utamlea kwa maadili mema kama hesima, kujituma, kusali na kupenda elimu sizani kama huyu mtoto ukubwani kwake atakupa shida sana, Tufike kipindi tuelewe umuhimu wa malezi bora kwa watoto wetu hakuna mtoto asiependa kupendwa kila mtoto anapenda mapenzi kutoka kwa wazazi wake wote pia mtoto anahuzunika kuona wazazi hawaelewani, mlinzi wa watoto niwewe na mimi tulio wazunguka kuwalinda kupo kwa aina nyingi unaweza kuta wanagombana ukasuruhisha, unaweza kuta wanacheza sehemu yenye hatari ukawatoa vile vile kuwavusha barabara, unakuwa umemtendea wema sana na ukimfanyia hivi mtoto atakupenda hadi ukubwani, ni jambo la aibu mtu mzima unakuta watoto wanagombana alaf ukapita tuu pembeni,

Pia kadri siku zinzvoenda watoto wa mitaani wanazidi kwa uchunguzi niliofanya sio kwamba wote ni yatima hawana ndugu, wengine wanandugu ila wameamua tu kukimbia makwao kutokana na sababu mbalimbali, kama upo hai unakubali vipi mwanao akimbie nyumbani akawe mtoto wa mtaani? hata kama hali nyumbani sio nzuri ila kama unaupendo huwez kukaa kuridhika na hili swala mwanao awe omba omba wewe umelala ndani,,

pia upande wa usafiri watoto wanapata tabu saaana utakuta madaftari mazito kakaastend mda mrefu, makonda  wameambiwa sana hii tabia ya unyanyasaji hawaelewi kwanini mimi na wewe pindi tukiona tusiwashitaki? serikali pia ingeweka magari mengi ya shule hizi za serikani naona magari ya shule mengi ni ya shule za matajiri, selikali yetu imeshindwa nini kuleta magari ya shule wakati wafasnyakaz wengi wa serikali wanao wanasoma shule za kulipia ndio zile zenye magari?


HIKI NI KILIO CHANGU kwa yoyote atakaesoma aone jinsi gani watoto wanapata shida sana jaman tuamke tuwalinde tuwatunze tuwasomeshe tuwape chakula MUNGU ATAWABARIKI SANA,
     WE ARE THE ONE WE ARE THE CHIDREN FROM ONE FATHER

1 comment:

  1. Thats nice Candy...it seems that una akili sana na una roho nzuri sana

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO HAPA