Thursday, February 28, 2013

CANDY:PAMOJA NA KUFANYA MUZIKI BADO NINANDOTO YA KUITANGAZA NCHI YANGU KIMITINDO


nachojua penye nia pana njia na ukikazana mafanikio yanakuja kwa wakati wake, nikiwa naendelea kuandika mashairi ya nyimbo zangu bado napanga mbinu nyingi za kukabiliana na mziki wa bongo, mwanzo nilipo anza rasmi kurecod haikuwa ngumu sana kwangu coz nilipokelewa vizuri kila studio niliofika na wamekuwa wakionesha mchango mkubwa kwangu kwa vitu vingi,.Kunakitu kina weza kukutokea katika maisha na ukakiwasilisha kwa jamii kwa njia ya muziki, mara nyingi napenda kuimba maisha yetu ya kawaida na mambo mengine ninayokumbana nayo nikiwa kama msichana.


natarajia kuachia nyimbo yangu karibuni na pia ntashukuru mungu endapo watanzania watanielewa na kunipokea kwani muziki bila mashabiki hakuna chochote waweza fanya, Japo muonekano wangu wengi wananishauri nifanye mitindo lakini mahisi sipo tayari kwa sasa japo napenda sana na naweza vitu vingi vinavohusu mitindo ila daima najua kila jambo linawakati wake . kwa mipango ya mungu nikija kufanikiwa kwenye muziki nina mpango wa kufungua kampuni yangu ya mitindo kwani ninauwezo wa kuchora nguo na kushona pia kudizaini vitu vingi vinavohusu urembo, Najua kwa kufanikisha hili nitaweza kuitangaza nchi yangu vizuri sana kitaifa na kimataaifa kupitia muziki na mitindo

pamoja na kujua kuimba bado ninauwezo mkubwa wa kudance aina nyingi za muziki wa mataifa mbalimbali pia nimejifunza mengi kuhusu dancing maana nategemea itanisaidia sana katika muziki wangu, 

 STAY TUNE FOR MA NEW SONG: PENZI LAKE

1 comment:

  1. We ril believe on your talent........keep it up candy we are praying for your success always

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO HAPA